Thursday 11 September 2014

Malinzi azindua Rock City Marathon 2014

Mratibu wa Rock City Marathon  kutoka kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi Grace Sanga (wa kwanza kulia) akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (Wa nne kulia) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi  wa Rock City Marathon 2014, jana jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baadhi ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za Rock City Marathon 2014 pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa riadha Tanzania, wakifuatilia yanayojiri wakati wa uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Msemaji wa Kampuni ya Capital Plus International, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, akizungumuza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF ) Bw. Jumanne Mbepo, ambao ndo wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano na mawasiliano wa TSN Group Koiya Kibanga, ambao ni moja wa  wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Na Mwandishi Wetu,
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, amezindua rasmi mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika Oktoba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema mbio hizo zimeweza kuwa ni moja ya mbio zinazoheshimika nchini Tanzania na kuiweka kanda ya ziwa katika kalenda ya michezo kila mwaka.
Malinzi aliipongeza kampuni ya Capital Plus International (CPI) kwa kuendelea kujidhatiti katika maandalizi ya mbio hizo na kuziboresha kila mwaka licha ya changamoto nyingi zinazoukabili mchezo huo wa riadha nchini.
 “Ni kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wamekuwa wakisaidia kukuza mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu unachangamoto nyingi.
“Jitihada za pamoja zinahitajika baina ya serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, sisi Baraza la Michezo la Taifa (BMT), vyama vya michezo, mashirika na wadau wengine, ili kurejesha heshima iliyopotea miongoni mwa michezo na wanamichezo wa Tanzania, hususani riadha,” alisema Bw. Malinzi.
Bw. Malinzi alibainisha kuwa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali CPI imekuwa ikijitahidi kuboresha mbio hizo zifanyikazo kila mwaka.
“Tumeshuhudia viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, ambapo ni kielelezo cha maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo wekwa,” aliongeza  Bw. Malinzi.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa BMT alisisitiza kuwa vyama vya michezo pia vinapaswa kujiimarisha katika kuwaandaa wachezaji kabla ya kuwapeleka kushiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo wachezaji hao wanabeba jina la nchi ya Tanzania.
“Hatunabudi kuimarisha msingi wetu katika kila aina ya michezo hapa nchini, kama bado tunayo ndoto ya kuirudisha ramani ya Tanzania katika ulimwengu wa michezo kama ilivyokuwa zamani,” alisisitiza.
Tukio hilo limewavutia wadau wengi wa michezo nchini, ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa kama Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya TSN Group Ltd, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), African Barrick Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF), Sahara Communication, ATCL, New Mwanza Hotel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza kudhamini mbio hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya Capital Plus International, Bw. Mathew Kasonta, alisema mbio za mwaka huu zitahusisha mbio za nusu Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha maarufu kama Corporate Race za kilomita 5, mbio za watu wenye ulemavu wa ngozi za kilomita 3, mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto kuanzia miaka saba hadi 10 ambazo ni za kilomita 2.
Bw. Kasonta alisema kuwa mbio hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo, ambapo washiriki watakua ni kutoka kanda ya ziwa Victoria na nchi jirani kama Kenya, Uganda, Afrika Kusini na baadhi yao wakiwa na uzoefu wa kucheza mashindano ya kimataifa ili kutoa ushindani zaidi.
“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafadhili mbalimbali wanaoshirikiana nasi ili kuyafanikisha mashindano haya, kwa niaba ya Capital Plus International, ningependa kuwahakikishia kuwa mashindano ya mwaka huu yataboreshwa zaidi na hivyo yataweza kutupatia wanariadha bora watakaoiwakilisha nchi yetu kikamirifu katika mashindano ya kimataifa,” alisema Bw. Kasonta.

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.